IQNA

Semina ya 'Nafasi ya Wanawake wa Kiislamu katika Kurekebisha Jamii' yafanyika Nigeria

17:18 - June 12, 2012
Habari ID: 2345406
Semina ya 'Nafasi ya Wanawake wa Kiislamu katika Kurekebisha Jamii' ilifanyika jana Jumatatu katika mji wa Buchi nchini Nigeria ambapo wanawake wa Kishia walishiriki.
Semina hiyo iliandaliwa na Kituo cha Kiislamu cha As'hab al Kisaa ambacho kinafungamana na Taasisi ya Thaqalain ya wanawake wa Kishia wa Nigeria.
Akiungumza kwenye semina hiyo, Fatuma Yunus mmoja wa wanaharakati mashuhuri wa kike wa Kiislamu katika mji huo aliwahutubia hadhirina kuhusiana na nafasi ya wanawake katika dunia pamoja na nafasi ya mwanamke wa Kiislamu katika kurekebisha jamii.
Mwishoni mwa semina hiyo Bibi Adama mmoja wa wahadhiri mashuhuri wa Kiislamu nchini Nigeria aliashiria nafasi ya athari hasi za teknolojia ya leo na hasa intaneti kwa malezi ya watoto na tabaka la vijana. 1027671
captcha