IQNA

17:58 - June 13, 2012
Habari ID: 2346230

Sherehe za kuadhimisha Dhaka kuwa mji mkuu wa kiutamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu kufanyika

Sherehe za kuadhimishwa Dhaka, mji mkuu wa Bangladesh kuwa mji mkuu wa kiutamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu katika mwaka huu wa 2012 zimepangwa kufanyika tarehe 14 Julai.

Kwa mujibu wa tovuti ya ISESCO, Muhammd Shafiq al-Islam, Katibu Mkuu wa Shirika la Utaalamu wa Mambo ya Kale atakutana leo Jumatano na Muhammad Nur al-Haq, Waziri wa Utamaduni wa Bangladesh ili kujadili mipango ya maadhimisho hayo.
Kila mwaka miji mikuu mitatu kati ya nchi za Asia, Afrika na ulimwengu wa Kiarabu huchaguliwa kuwa miji mikuu ya utamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu. Katika kipindi chote ambapo miji hiyo huchaguliwa kuwa miji mikuu ya kiutamaduni ya ulimwengu wa Kiislamu katika maeneo yao, hutakiwa kuandaa na kutekeleza ratiba toafauti za Kiislamu kwa lengo la kuhuisha utambulisho wa Kiislamu.
Katika mwaka huu wa milaadi, miji mitatu ya Najaf nchini Iraq, Dhaka Bangladesh na Niamey nchini Niger imechaguliwa kuwa miji mikuu ya kiutamaduni ya ulimwengu wa Kiislamu. 1029090
captcha