IQNA

Adhabu ya wanaovunjia heshima matukufu ya kidini kuainishwa Tunisia

13:52 - June 14, 2012
Habari ID: 2346584
Timu ya chama cha Kiislamu cha an Nahdha katika Baraza la Kitaifa la Waasi nchini Tunisia limetaka kuwekwe kifungu kinachoainisha adhabu ya watu wanaovunjia heshima matukufu ya kidini katika katiba mpya ya nchi hiyo.
Chama cha an Nahdha kimetoa ombi hilo baada ya kushadidi malalamiko dhidi ya mabango yanayovunjia heshima matukufu ya Kiislamu katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis.
Taarifa ya chama hicho imesema kuwa matukufu ya kidini yana nafasi maalumu na hayapaswi kuvunjiwa heshima kwa vitendo visivyo na thamani.
An Nahdha imesisitiza kuwa japokuwa chama hicho kinaunga mkono uhuru wa kusema na kujieleza lakini haupasi kutoka nje ya mipaka na kanuni na wale wote wanaodai kutetea uhuru huo wanapaswa kuheshimu itikadi za taifa la Tunisia.
Taarifa hiyo pia imevitaka vyombo vya sheria kufanya uchunguzi na kuwahukumu waliovunjia heshima matukufu ya kidini na kuharibu mali ya umma. 1029014
captcha