IQNA

Iran yawakamata waliohusika na mauaji ya wanasayansi wake wa nyuklia

14:45 - June 16, 2012
Habari ID: 2347717
Wizara ya Usalama wa Taifa ya Iran imetangaza kuwa vyombo vya usalama vimewatia nguvuni watu waliohusika na mauaji ya wanasayansi wa nyuklia hapa mjini Tehran mwaka huu na mwaka 2010.
Taarifa ya Wizara hiyo imesema uchunguzi mkali uliofanywa na vitengo kadhaa vya usalama umepelekea kukamatwa watu hao ambao kwa sasa wanashikiliwa huku wakiendelea kusailiwa. Waliokamatwa wamekiri kuwa na mfungamano na utawala haramu wa Israel.
Mostafa Ahmadi Roshan, mwanasayansi wa nyuklia wa hapa Iran aliuawa mwezi Januari mwaka huu baada ya bomu kutegwa kwenye gari lake.
Novemba mwaka 2010 mtaalamu mwingine wa nyuklia hapa nchini, Prof. Majid Shahriari aliuawa baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.
1030240
captcha