Ayatullah Ahmad Jannati amekumbusha kwamba Iran imepitia kipindi kigumu cha uchokozi kutoka kwa dikteta wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein aliyekuwa akiungwa mkono na Wamagharibi na pia vikwazo vya zaidi ya miaka 30 vya Marekani na kwa mantiki hiyo nchi hii haiwezi tena kutishwa wala kubabaishwa na yeyote.
Akizungumzia mazungumzo yajayo kati ya Iran na kundi la 5+1, Ayatullah Jannati amesema Iran itaingia kwenye mazungumzo hayo na mtazamo wa ushirikiano na wala sio kuwapigia magoti Wamagharibi. Amesisitiza kuwa takwa la Iran ni kuheshimiwa haki yake ya kurutubisha urani kwa malengo ya amani kwa mujibu wa sheria za Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA. Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika Juni 18 na 19 mjini Moscow, Russia.
1030379