IQNA

Mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia aaga dunia

23:51 - June 16, 2012
Habari ID: 2348028
Idara ya Kasri ya Ufalme wa Saudi Arabia imetangaza kuwa, mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo Nayif bin Abdul Aziz amefariki dunia leo mjini Geneva, Uswisi alikokuwa amekwenda kwa ajili ya matibabu.
Habari zaidi zinasema kuwa, Nayif bin Abdul Aziz amefariki dunia kwa ugonjwa wa kansa uliokuwa unamsumbua kwa muda mrefu. Al Amir Nayif bin Abdul Aziz alichaguliwa katika cheo hicho tarehe 18 Oktoba 2011 akiwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani.
Kifo hicho kinatarajiwa kuzusha vita vya ndani vya kuwania madaraka katika nchi hiyo. Waledi wa mambo wanamtaja Nayif kuwa alikuwa mwenye mielekeo mikali kumzidi mfalme Abdullah bin Abdul Aziz.
Aidha Nayif bin Abdul Aziz atakumbukwa kwa kumkaribisha aliyekuwa rais wa Tunisia Zine El Abidine Ben Ali na kutuma vikosi vya nchi hiyo Bahrain kwa lengo la kuyateka nyara mapinduzi ya wananchi wa nchi hiyo wanaodhulumiwa kila uchao.
captcha