IQNA

Mashia wa Finland kuadhimisha uzawa wa Imam Hussein (as)

16:25 - June 17, 2012
Habari ID: 2348814
Waislamu wa Finland wanapanga kuadhimisha siku ya uzawa wa Imam Hussein (as) hapo siku ya Alkhamisi Juni 21.
Maadhimisho hayo ambayo yatahudhuriwa na Hujjatul Islam wal Muslimin Naqawiyan, msomi na mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu yameandaliwa na Kituo cha Kiislamu cha Ujumbe wa Ahlul Beit (as).
Maadhimisho hayo yatakayofanyika katika Msikiti wa Fatma az-Zahra pia yatajumuisha ratiba za kusherehekea kubaathiwa Mtume Mtukufu (saw) aliyeoongoza wanadamu katika njia nyoofu na ya saada humu duniani na huko Akhera.
Kituo cha Kiislamu cha Ujumbe wa Ahlul Beit (as) kwa anwani ya www.resalat.fi ni kituo pekee rasmi cha Kishia nchini humo. Mwaka uliopita kituo hicho kilifungua msikiti wa kwanza wa Kishia mjini Helsinki kwa jina la Bibi Fatma (as), kwa mnasaba wa kuzaliwa Bibi huyo mtukufu wa Uislamu. 1029313
captcha