IQNA

Askari wa zamani wa Israel kujiunga na mapambano ya Wapalestina

17:41 - June 17, 2012
Habari ID: 2348863
Askari mmoja wa zamani wa Israel ametangaza kuwa anataka kutupilia mbali uraia wa Israel na kuhamia katika mojawapo ya kambi za wakimbizi wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi.
Kanali ya Televisheni ya Press imetangaza kuwa Andre Pishanichikov mwenye umri wa miama 23 ambaye ni Myahudi kutoka Tajikistan, amesema anataka kuhamia katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya al Dahisa katika eneo la Bait Laham ambako alikuwa akiishi kama kibarua na mjenzi wa nyumba. Andre Pishanichikov ambaye kwa sasa yuko safarini barani Ulaya amesema ana nia ya kuhamia Palestina.
Pishanichikov alianza kukosoa siasa za utawala wa Kizayuni wa Israel wakati alipokuwa akihudumu katika jeshi la utawala huo ghasibu. Ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba anachukia uzayuni na anataka kujiunga na mapambano ya uhuru ya wananchi wa Palestina. 1032055

captcha