Kanali ya televisheni ya Press imemnukuu Sarah Flanders akisema kuwa hii leo Marekani ndiye mkiukaji mkuu wa haki za binadamu duniani ndani ya nchi na katika medani ya kimataifa.
Kituo cha The International Action Center (IAC) kinakusanya pamoja wanaharakati wanaopinga vita na siasa za kibepari za Marekani.
Flanders amesema kuwa harakati ya kuteka Wall Street ni mfano wa yale yanayotendeke mara kwa mara nchini Marekani.
Amesema kutiwa mbaroni kwa wingi watu wasiokuwa na hatia, kutolewa taswira isiyokuwa sahihi kuhusu vyombo vya habari na kuwatambua vijana wanaopigania haki zao kuwa ni wahalifu ni mifano ya wazi ya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na serikali ya Marekani. 1034438