Sayyid Sadruddin al Qubanchi aliyekuwa akihutubia katika Husainiya ya Fatimiyya mjini Najaf amesema kuwa utawala uliopotoka wa Saudia unapaswa kubadilika katika zama hizi za mwamko wa mataifa mbalimbali.
Ameongeza kuwa Mashia na Masuni wa Saudia wamechoshwa na utawala wa kiimla wa Riyadh na wanahitaji msaada.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, hatibu wa Sala ya Ijumaa ya Najaf amegusia mgogoro wa sasa wa Syria na kusema kunashuhudia misimamo ya kindumakuwili dhidi ya nchi hiyo na makundi ya upinzani yanasaidiwa na nchi za kigeni.
Amesema kuwa wapinzani wa serikali ya Syria wanasaidiwa ya nchi za nje huku wananchi wa Bahrain wakiendelea kunyanyaswa na utawala wa nchi hiyo na kupuuzwa na jumuiya za kimataifa. Amesema jeshi la Ngao ya Kisiwa ambalo Saudia ni mwanachama wake pia limepelekwa Bahrain kuwakandamiza wanamapinduzi wanaopigania haki zao za kiraia. 1040943