IQNA

Zaidi ya watu 40 wauawa kwenye milipuko ya mabomu nchini Iraq

20:06 - July 03, 2012
Habari ID: 2360380
Habari kutoka Iraq zinasema kuwa zaidi ya watu 40 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa kwenye milipuko ya mabomu katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo.
Watu 40 wameuawa mjini Diwaniya yapata kilomita 180 kusini mwa Baghdad huku wengine 4 wakiuawa katika mji mtakatifu wa Karbala. Mlipuko wa Diwaniya umetokea katika soko la watu wengi na imeripotiwa kwamba lori lililokuwa limesheheni mada za milipuko ndilo lililosababisha maafa hayo.
Katika mji wa Karbala gaidi mmoja alijiripua katikati ya umati wa Waislamu wa madhehebu ya Shia. Polisi imesema huenda idadi ya vifo ikapanda kwani majeruhi wengi wako katika hali mahututi.
Milipuko hiyo imetokea wakati Waislamu kote ulimwenguni hususan wafuasi wa madhehebu ya Shia wakijitayarisha kwa ajili ya sherehe za siku ya kuzaliwa mwokozi anayesubiriwa, Imam wa Zama Mahdi (as) inayozadifiana na Alhamisi ijayo. 1044357
captcha