IQNA

Makanisa ya Marekani yaunga mkono ujenzi wa msikiti St. Anthony

20:57 - July 07, 2012
Habari ID: 2362845
Wanachama wa makanisa matatu ya jimbo la Minnesota huko Marekani wamechukua uamuzi wa kuitisha mkotano kesho Jumapili kwa shabaha ya kupambana na propaganda chafu dhidi ya Uislamu zinazofanywa na Baraza la Mji St. Anthony.
Mkutano huo pia utapinga hatua ya baraza la mji huo ya kupiga marufuku ujenzi wa msikiti katika mji huo.
Kituo cha On Islam kimeripoti kuwa Elisa Marty ambaye ni miongoni mwa wasimamizi wa mkutano huo amesema kuwa utafanyika kwa lengo la kuunga mkono jamii ya Waislamu wa mji wa St. Anthony na kudhihirisha mfungamano wa Wakristo wa mji huo na Waislamu.
Ameongeza kuwa Wakristo wa St. Anthony wanataka kuonesha kwamba hali ya mambo ni kinume na uamuzi wa baraza la mji huo na kwamba wana uhusiano mzuri na wafuasi wa dini mbalimbali.
Mkutano huo utahutubiwa na Wakristo na wanazuoni wa Kiislamu kuhusu utambuzi wa dini mbalimbali na maelewano kati ya wafuasi wa dini hizo.
Mwezi uliopita Baraza la Mji wa St. Anthony lilipinga mpango wa ujenzi wa msikiti wa Waislamu katika mji huo. Kabla ya uamuzi huo kundi moja la wakazi wa mji huo lilivunjia heshima matukufu ya Kiislamu na kutangaza kwamba linapinga ujenzi wa eneo la ibada kwa ajili ya Waislamu.
Baada ya matukio hayo viongozi wa Waislamu wa St. Anthony wameanzisha harakati za kisheria za kuruhisiwa ujenzi wa msikiti.
Katika miezi ya hivi karibuni kumejitokeza wimbi kubwa la upinzani wa ujenzi wa misikiti na maeneo ya ibada ya Waislamu katika miji mbalimbali ya Marekani. Mipango ya ujenzi wa misikiti karibu 35 imekwamishwa huko Marekani na misikiti kadhaa ya Waislamu nchini humo imeharibiwa. 1046863




captcha