IQNA

Kongamano la kumuenzi Fadhlullah kufanyika kesho Pakistan

23:01 - July 07, 2012
Habari ID: 2362880
Kongamano la kumuenzi mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu Ayatullah Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah ambaye alikuwa miongoni mwa maraji wakubwa wa Waislamu wa madhehebu ya Shia limepangwa kufanyika kesho mjini Karach, Pakistan chini ya usimamizi wa jumuiya ya Darul Hidaya al Islamiyya.
Mwandishi wa IQNA huko mashariki mwa Asia ameripoti kuwa kongamano hilo litafanyika katika ukumbi wa Behujani likihudhuriwa na shakhsia wa kielimu na wasomi wa Pakistan.
Miongoni mwa watakaohutubia kongamano hilo ni Hujjatul Islam Baqir Zaidi, Ustadh Shahis Kashifi na Sayyid Muhammad Ali naqawi.
Allama Fadhlullah alizaliwa mwaka 1935 katika mji wa mtakatifu wa Najaf nchini Iraq katika familia ya kidini yenye asili ya Lebanon. Allama Muhammad Hussein Fadhlullah alianza kujifunza elimu ya dini katika Hauza ya kielimu ya mji wa Najaf tangu akiwa kijana. Ayatullah Fadhlullah alijishughulisha na masuala ya kutwalii makala na kuandika vitabu na alikuwa na nafasi muhimu katika kuasisi harakati ya kisiasa huko Iraq iliyojulikana kwa jina la "Hizbul Da'awa al Islamiya". Mwaka 1966 baadhi ya wananchi na maulamaa wa Lebanon walimwalika nchini humo Allama Fadhlullah na akiwa huko alifanya kazi kubwa za kielimu, kiutamaduni na kijamii, shughuli ambazo athari zake zinaendelea kushuhudia hadi leo hii.
Allama Muhammad Hussein Fadhlullah alikuwa miongoni mwa waungaji mkono wakubwa wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na harakati ya Muqawama wa kiislamu ya Lebanon Hizbullah na sababu hiyo ndiyo iliyokuwa ikizikasirisha Marekani na utawala wa Kizayuni na kupelekea kiongozi huyo kukoswakoswa kuuawa kwa mara kadhaa.
Ayatullah Sayyid Muhammad Husseinn Fadhlullah ameandiak vitabu vingi vya thamani ikiwemo tafsiri yenye juzuu 25 kwa jina la "Min Wahyil Qur'an."
captcha