Kwa mujibu wa gazeti la al-Watan linalochapishwa nchini Saudia Sheikh Abdallah Rajab amekuwa akiadhini kwenye msikiti huo kwa zaidi ya miaka 50. Alizikwa siku ya Jumamosi katika makaburi ya Baqii baada ya kuswaliwa swala ya maiti katika Msikiti wa Mtume (saw).
Sheikh Abdullah Rajab alizaliwa mwaka 1348 Hijiria katika mji wa Madina na kupata masomo yake katika mji huohuo. Aliteuliwa kuwa mwadhini rasmi wa msikiti huo mwaka 1385.
Kabla ya kuwekwa mitambo ya kisasa ya sauti kwenye msikiti huo, Abdullah Rajab alikuwa akiadhini kupitia minara ya msikiti huo lakini baada ya kupatwa na maradhi adhana yake imekuwa ikisikika nyakati za asubuhi tu. 1047449