Kituo cha habari cha On Islam kimeripoti kuwa kwa mujibu wa sensa hiyo jamii ya Waislamu wa San Diego imeongezeka kwa asilimia 179 tangu mwaka 200 hadi 2010.
Sensa hiyo inaonesha kuwa idadi ya Waislamu katika mji huo imeongezeka kutoka watu 7878 hadi 21994. Sensa hiyo pia imeonesha kuwa Uislamu unashika nafasi ya saba kwa kuwa na wafuasi wengi huko San Diego.
Sensa hiyo imefanywa na Jumuiya ya Takwimu za Taasisi za Kidini kwa lengo la kuainisha idadi ya makundi ya kidini na kuhesabu maeneo ya ibada katika mji huo.
Wahajiri Waislamu kutoka nchi kama Somalia, Iraq, Afghanistan na Bosnia na kuongezeka idadi ya misikiti katika mji huo kumetajwa kuwa ni miongoni mwa sababu za kustawi kwa haraka dini ya Uislamu katika mji wa San Diego. 1048252