Katika muswada huo chama cha Uadilifu na Ustawi kimesema, kwa kutilia maanani vipengee vya 14, 16 na 24 vya katiba vinavyohusu masuala ya elimu na uhuru wa mtu binafsi katika jamii kuna matarajio kwamba kutafanyika mabadiliko ya dharura na kufutwa marufuku ya vazi la hijabu nchini Uturuki.
Wawakilishi wa chama hicho wametaka kufanyike mabadiliko makubwa katika katiba ya Uturuki na kufutwa marufuku ya vazi la hijabu na marufuku ya kutolewa masomo ya dini ya Kiislamu katika shule za nchi hiyo.
Wanawame na wasichana wa Kiislamu nchini Uturuki wamekuwa wakipinga vikali marufuku ya vazi la hijabu iliyowekwa na watawala wa kisekulari wa serikali ya zamani ya nchi hiyo. Wanafunzi wa kike wanaovaa vazi la Kiislamu la hijabu wanazuiliwa kusoma katika vyuo vikuu vya Uturuki. 1049635