IQNA

Wanaharakati wa kisiasa waandamana mbele ya ubalozi wa Saudia, London

19:20 - July 10, 2012
Habari ID: 2365478
Makundi ya wanaharakati wa madhehebu ya Kiislamu ya Shia na wale wa masuala ya kisiasa wameandamana leo mbele ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini London, Uingereza wakipinga hatua ya utawala wa kifalme wa Riyadh ya kumtia nguvuni Sheikh Ayatullah Baqir Nemr al-Nemr.
Wanaharakati wa kisiasa wa Saudia walipinga vikali kitendo cha askari usalama wa Saudi Arabia cha kumtia nguvuni Ayatullah Nemr na kuua raia watatu katika maandamano ya amani yaliyofanyika katika mkoa wa Qatif huko mashariki mwa Saudia.
Waandamani hao waliutaja utawala wa Aal Saud kuwa ni wa kidikteta, wa kigaidi na unaofanya mauaji dhidi ya watu wasiokuwa na hatia na wametoa wito wa kukomeshwa ukiukaji wa haki za binadamu nchini Saudi Arabia.
Waandamanaji hao wa London wamekemea kimya cha nchi za Magharibi na jumuiya za kutetea haki za binadamu za kimataifa mbele ya ukandamizaji na mauji yanayofanywa dhidi ya watu wanaofanya maandamano ya amani nchini Saudia na wametaka Sheikh Nemr al-Nemr aachiwe huru mara moja.
Watu watatu walipigwa risasi na kuuawa na vikosi vya Saudia Arabia katika maandamano yaliyofanyika Jumapili iliyopita katika mji wa Awwamiyya huko mashariki mwa Saudia kupinga kitendo cha kutiwa nguvuni Sheikh Nemr al Nemr. 1049316
captcha