IQNA

Al Azhar yasisitiza sheria za Kiislamu zitawale Misri

17:34 - July 12, 2012
Habari ID: 2366901
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al Azhar cha Misri ametoa taarifa na kusisitiza kuhusu udharura wa kutimika sheria za Kiislamu kama msingi wa katiba mpya ya Misri.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katika taarifa iliyotolewa Julai 11 , Sheikh Ahmad Tayyib ambaye ni Sheikhe Mkuu wa Al Azhar amesema: 'Sisi tunapinga kuongezwa au kupunguzwa vipengee katika sehemu ya pili ya katiba ya Misri inayosisitiza kuhusu misingi ya Kiislamu katika sheria za nchi.'
Sheikh Ahmad Tayyib ameongeza kuwa sheria za Kiislamu zinapaswa kuzingatiwa kama chanzo cha sheria katika katiba mpya. Ameongeza kuwa dini rasmi ya Misri ni Uislamu nayo lugha rasmi ni Kiarabu na msingi wa utungaji sheria ni mafundisho ya Kiislamu.
Sheikul Azhar ameongeza kuwa Chuo Kikuu cha Al Azhar lina jukumu la kisheria, kitaifa na kihistoria na kwa hivyo ataendelea kutetea suala la Uislamu kuwa chanzo cha sheria za Misri.
1050609
captcha