IQNA

Waislamu wa Myanmar wakandamizwa

11:18 - July 14, 2012
Habari ID: 2367336
Serikali ya Myanmar inawakandamiza Waislamu waliowachache wa kabila la Rohingya na sasa ambao wametimuliwa kutoka eneo lao la jadi.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa Waislamu wa Myanmar ni kati ya watu wanaokandamizwa zaidi duniani.
Antonio Guterres Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi UNHCR amesema shirika hilo linawapa misaada wakimbizi Waislamu na kujaribu kuwarejesha katika maeneo yao ya asili.
Tokea mwezi Juni mwaka huu wa 2012, mamia ya Waislamu wa kabila la Rohingya wameuawa na makumi ya maelfu ya wengine kuachwa bila makao kufuatia machafuko yaliyozuka mashariki mwa Myanmar. Idadi ya Waislamu wa kabila la Rohingya ni karibu milioni moja kati ya watu milioni 47 nchini Myanmar.
Juni 3 Waislamu 10 wa kabila la Rohingya waliuawa na genge la Mabuddha lijulikanalo kama Rakhines. Mashirika ya kutetea haki za binaadamu yanasema kutoka Juni 10-28 Waislamu 650 wa kabila la Rohingya waliuawa, 1,200 wametoweka na hawajulikani waliko na wengine 80,000 wameachwa bila makao. Jeshi la Myanmar linalaumiwa kwa kuongoza kampeni ya kuwakandamiza Waislamu.
Myanmar ambayo zamani ikijulikana kama Burma ni nchi iliyo kusini mashariki mwa Asia na inapakana na India, Bangladesh, China, Laos na Thailand.
1051605
captcha