Marwan Muhammad ambaye ni mwanachama wa jumuiya ya kupiga vita propaganda chafu hidi ya Uislamu ameiambia Press TV kwamba jinai zinazotokana na chuki na uhasama dhidi ya Waislamu zimeongezeka nchini Ufaransa kwa sababu baadhi ya wahalifu wamejihisi kupata nguvu zaidi katika miaka ya hivi karibuni.
Amesema kunashuhudiwa ongezeko la jinai dhidi ya Waislamu na kwamba asilimia 92 ya wahanga wa jinai hizo ni wanawake.
Maafisa usalama wa viwanja vya ndege vya Ufaransa pia wamekuwa wakiwavua vazi la hijabu wanawake wa Kiislamu mbele ya umati kwa kutumia kisingizio cha kulinda usalama.
Kitendo hicho kinakiuka sheria za usalama katika viwanja vya ndege za Umoja wa Ulaya ambazo zinasisitiza kuwa maafisa usalama hawana haki ya kuwataka wanawake wa Kiislamu kuvua vazi lao la hijabu. 1052922