Hayo ni kwa mujibu wa qarii wa Qur'ani kutoka Ubelgiji Ibrahim al Hashemi ambaye katika mahojiano na IQNA amesema, 'nilishiriki katika Mashindano ya Tatu ya kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu yaliyofanyika Iran mwaka 2011 na nilishuhudia ukarimu, umoja na mshikamano wa watu wa Iran.'
Qarii huyo amesema kuna umuhimu wa kutafakari kuhusu aya za Qur'ani Tukufu na kuongeza kuwa ili kufikia kiwango cha juu katika suala hili, kuna hataja ya kuzitafakari aya kwa nidhamu maalumu. Qari al Hashemi amesema Qur'ani Tukufu ndio kimbilio muafaka na bora zaidi wakati mwanadamu anapokosa matumaini na kukumbwa na masaibu.
Ameendelea kusema kuwa Qur'ani ina nafasi muhimu katika kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu.
Mashindano ya 4 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu kwa ajili ya Wananchuo Waislamu yanatazamiwa kufanyika Septemba 12 na 15 katika mji wa Tabriz kaskazini magharibi mwa Iran.
Mashindano hayo huandaliwa Shirika la Harakati za Qur'ani la Wanachuo wa Iran kwa lengo la kuinua kiwango cha harakati za Qur'ani na kuleta umoja na ushirikiano kwa msingi wa Qur'ani miongoni mwa Waislamu wanafunzi wa vyuo vikuu kote duniani.
1053189