IQNA

Rais wa Iran awasihi Waislamu kukata uhusiano wowote na Israel

12:58 - September 15, 2025
Habari ID: 3481234
IQNA – Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amezitaka nchi za Kiislamu kukata kabisa uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel, kabla ya mkutano wa dharura utakaofanyika Doha kufuatia shambulizi la hivi karibuni la Israel dhidi ya Qatar.

Viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu wanakusanyika mjini Doha Jumatatu hii kwa ajili ya mkutano wa kipekee unaoandaliwa na Qatar. Mkutano huu unakuja siku chache baada ya utawala wa Kizayuni Israel kutekeleza shambulizi lake la kwanza kwenye ardhi ya Qatar, likilenga viongozi wakuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas.

Shambulizi hilo liliua baadhi ya ndugu na wasaidizi wa viongozi hao, lakini lilishindwa kuua uongozi wa kundi hilo. Hatua hii imepokelewa kwa kulaani kote kwenye kanda hii. Akizungumza Tehran kabla ya kuondoka kuelekea kwenye mkutano Jumatatu, Rais Pezeshkian amesema kuwa Israel "haina mipaka wala muundo wa vitendo vyake" na alionya kuwa nchi kama Lebanon, Syria, Qatar, Iran, Yemen, na Iraq ziko hatarini kukumbana na mashambulizi kama haya.

Aliongeza kuwa "Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya kwa bahati mbaya zinaziunga mkono vitendo hivi vya unyanyasaji." Rais wa Iran alielezea hali ya Gaza kama janga la kibinadamu. "Ukatili wa kimbari unafanyika," alisema, akionyesha kwamba wanawake, watoto, na wazee wanakufa kutokana na njaa na mashambulizi ya anga. Alisema kuwa Marekani imeiwezesha Israel kutekeleza  jinai kupitia "veto au kura yake ya turufu  katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na msaada wake kwa utawala wa ubaguzi wa rangi."

Rais Pezeshkian amesisitiza kwamba mkutano huu leo Doha unapaswa kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za Kiislamu. "Lengo letu kuu ni kuongeza umoja na mshikamano ili tuweze kuchukua hatua kwa nguvu kwenye majukwaa ya kisheria na mashirika ya kimataifa dhidi ya utawala huu," alisema.

Alieleza kuwa ikiwa nchi za Kiislamu zitashirikiana, zinaweza kuchukua hatua halisi katika "nyanja za kiuchumi, kitamaduni, kijamii, na mawasiliano" na hatimaye kukata uhusiano na Israeli. "Ikiwa Waislamu wakiungana," aliongeza, "utawala wa Kizayuni hautathubutu kushinikiza nchi za Kiislamu au kuvunja sheria za kimataifa kirahisi."

3494608

captcha