IQNA

Mwezi Mwekundu kuonekana duniani, Waislamu wataswali swala maalumu

14:39 - September 07, 2025
Habari ID: 3481191
IQNA – Usiku wa tarehe 7 hadi 8 Septemba 2025, tukio nadra la kupatwa kwa mwezi kwa jumla, linalojulikana kama Mwezi Mwekundu, litaonekana katika maeneo mengi duniani. Tukio hili la kiasili litaambatana na kuswaliwa kwa swala maalumu ijulikanayo kama Sala ya Ayat na Waislamu katika sehemu mbalimbali.

Huko Najaf, Iraq Ofisi ya Ayatollah Mkuu Ali al-Sistani imetangaza kuwa kupatwa kwa mwezi kutaanza saa 12:28 jioni, kufikia kilele saa 3:11 usiku, na kumalizika saa 5:55 usiku kwa saa za eneo hilo. Tukio hili litaonekana kwa uwazi katika miji yote ya Iraq.

Katika mji wa Tehran, Iran, Taasisi ya Jiografia ya Chuo Kikuu cha Tehran imesema kupatwa kutaanza saa 1:57 jioni, na mwezi kufunikwa kabisa kuanzia saa 3:01 hadi 4:23 usiku kwa saa za eneo. Tukio litaisha saa 5:27 usiku na litaonekana kote nchini.

Swala ya Ayat 

Wanazuoni wa Kiislamu wameeleza kuwa Salat al-Ayat ni Sunnah thabiti ya Mtume Muhammad (SAW), inayoswaliwa mtu mmoja mmoja au kwa jamaa wakati wa matukio ya kiasili au kimaumbile kama kupatwa kwa mwezi au jua. Swala hii ina rakaa mbili, na Mtume (SAW) aliswali mwenyewe katika matukio kama haya.

Huko Misri Wizara ya Wakfu imetangaza kuwa swala maalumu itaswaliwa katika misikiti mikuu kote nchini usiku huu, kwa lengo la kufufua Sunnah ya Mtume Muhammad (SAW). Kituo cha Kimataifa cha Fatwa cha Al-Azhar kimehimiza umuhimu wa swala hii ambayo pia hukulikana kam Salatu Kusuf na kuwakumbusha waumini wasichelewe kuswali hadi mwezi uanze kuonekana tena.

Maeneo Yatakayoona Tukio Kupatwa kwa mwezi kutakuwa miongoni mwa matukio yanayoonekana kwa upana zaidi katika miaka ya hivi karibuni. Takriban asilimia 85 ya watu duniani wataweza kushuhudia angalau sehemu ya tukio hili. Asia, Afrika Mashariki, Asia Magharibi (Mashariki ya Kati), Ulaya, na Australia zitapata

Mwezi Mwekundu

Katika awamu ya kupatwa kwa jumla, mwezi utachukua rangi nyekundu kutokana na mwanga wa jua kupita katika angahewa ya dunia. Hili ni jambo linalofanya tukio hili kuitwa Mwezi Mwekundu. Awamu hii itadumu kwa zaidi ya dakika 80.

Mwezi wa Mahindi Kwa baadhi ya jamii za Amerika Kaskazini, mwezi huu wa Septemba hujulikana kama Corn Moon, ukionyesha msimu wa mavuno.

4303715

captcha