Kesi hiyo inawahukumu baadhi ya shakhsia wakubwa wa utawala wa kidikteta wa Muammar Gaddafi akiwemo binamu yake Ahmad Ibrahim ambaye ndiye mnadharia wa Kitabu cha Kijani (Green Book), mkurugenzi wa kikosi maalumu cha Gaddafi kilichokuwa maarufu kwa jina la Gadi ya Wananchi Mansour Dhoo na Mufti Mkuu wa utawala wa Gaddafi Khalid Tantus.
Kesi hiyo inafanyika siku kadhaa baada ya shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch kukosoa hali mbaya ya mahabusu wanaoshikiliwa katika jela za Libya.
Libya pia inajitayarisha kumfungulia kesi mwana wa kiume wa dikteta wa zamani wa nchi hiyo, Seiful Islam ingawa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) inataka akahukumiwe huko The Hague. 1055588