IQNA

Watoto 700 wa Uturuki watunukiwa nakala za Qur'ani

21:20 - July 17, 2012
Habari ID: 2371220
Jumuiya ya Reyhan-Der ya Uturuki imewatunuku watoto 700 nakala za Qur'ani Tukufu katika mji wa Merzifon katika mkoa wa Amasya kwa mnasaba wa kukaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Muammer Sarıkaya amesema kuwa watoto wa mji huo hushiriki kwa wingi katika misikiti na shule za kufunza Qur'ani Tukufu katika kipindi cha kiangazi na katika njia hiyo husaidiwa na familia, jumuiya na taasisi mbalimbali za Kiislamu. Amesisitiza kuwa jumuiya yake pia imechukua hatua ya kutoa nakala za Qur'ani kwa watoto 700 wa mji wa Merzifon kwa lengo la kuwahamasisha watoto kujifunza na kusoma Qur'ani Tukufu.
Muammer Sarıkaya ameongeza kuwa familia na viongozi wote wanawatakia mafanikio na ufanisi watoto wao na kwa msingi huo kuna udharura wa kuthamini mahudhurio yao katika darsa za Qur'ani kwa kutumia mbinu mbalimbali na kuwaenzi watu wanaotoa huduma katika njia hiyo. 1055704
captcha