Kwa mujibu wa gazeti la nchi hiyo la as-Sabil, Gassan az-Zuweidi mkurugenzi mratibu wa zawadi hiyo amesema mashindano hayo yaliyowashirikisha wasomaji bora wa Qur'ani kutoka mikoa yote ya Jordan yatapeperushwa hewani kupitia vyombo vilivyotajwa vya habari katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Amesema lengo la kuandaliwa mashindano hayo ni kujaribu kutafuta watu walio na vipawa vya usomaji Qur'ani miongoni mwa Wajordan ambapo 100 kati ya hao tayari wamefanikiwa kuingia katika duru ya mwisho ya mashindano hayo ambayo itafanyika mwishoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Amesema mshindi wa kwanza atazawadiwa gari. Waandaaji wa mashindano hayo wamesema lengo jingine ni kuhudumia Qur'ani na kuwaandaa wasomaji wa nchi hiyo waweze kushiriki katika mashindano ya kitaifa na kimataifa ya Qur'ani Tukufu. 1055199