IQNA

Waziri wa Ulinzi wa Syria auawa katika shambulizi la kigaidi

17:38 - July 18, 2012
Habari ID: 2372127
Waziri wa Ulinzi wa Syria Daoud Rajha ameuawa leo katika shambulizi la kigaidi lililolenga jengo la Usalama wa Taifa mjini Damascus.
Shambulizi hilo la kigaidi limetokea wakati baadhi ya mawaziri wa serikali na makamanda wa ngazi za juu wa jeshi walipokuwa katika mkutano kwenye jengo hilo.
Televisheni ya al Alam imeripoti kutoka Syria kwamba shambulizi hilo la kigaidi limetekelezwa na mmoja wa walinzi wa eneo mkutano huo ulipokuwa ukifanyika na kwamba Naibu Mkuu wa Majeshi ya Syria Assef Shawkat pia ameuawa katika shambulizi hilo.
Maafisa kadhaa wa ngazi za juu akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani Mohammad Ibrahim al-Shaar na Naibu Waziri Mkuu wa Syria pia wamejeruhiwa. Hali ya baadhi ya majeruhi imeripotiwa kuwa ni mbaya sana.
Takwimu kamili za maafisa waliouawa na kujeruhiwa katika shambulizi hilo bado hazijatolewa lakini inatabiriwa kuwa shambulizi hilo la kigaidi limeua na kujeruhi watu wengi.
Magaidi wanaosaidiwa na nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani na Israel pamoja na baadhi ya nchi za Kiarabu kama Saudi Arabia na Qatar wamezidisha mashambulizi kama hayo ya kigaidi nchini Syria katika siku chache za hivi karibuni. 1056787





captcha