IQNA

Mashindano ya Qur'ani kufanyika Tanzania

14:40 - July 21, 2012
Habari ID: 2373759
Mashindano ya Qur'ani Tukufu yamepangwa kufanyika kesho Jumapili Ramadhani Pili katika Medani ya Mwembe Chai katika mtaa wa Temeke mjini Dar es Salaam kwa mnasaba wa kuwadia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Mashindano hayo ambayo yameandaliwa na Madrasa ya Nyota yatahudhuriwa na wanafunzi 400 ambao watagawanywa katika makundi mawili ya wanawake na wanaume. Washindani watachuana kusoma na kuhifadhi aya na sura za Qur'ani Tukufu katika mashindano hayo ambayo yamepangwa kuanza kesho saa tatu asubuhi kwa wakati wa Afrika Mashariki na kumalizika kabla ya swala ya adhuhuri. 1058097
captcha