Mzee huyo mwenye umri wa miaka 65, aitwaye Albert, alitangaza kuingia kwake katika dini ya Kiislamu baada ya kutamka Shahada (tamko la imani linalosema: “Hakuna mungu isipokuwa Allah, Muhammad ni Mtume wa Allah”) mbele ya kundi la waumini waliokusanyika katika Msikiti Mkuu wa Mina, kwa mujibu wa tovuti ya Al-Tariq.
Albert aliamua kubadilisha mwelekeo wa maisha yake na kuanza awamu mpya kwa jina la Muhammad.
Hatua hiyo ilitokea sambamba na siku yake ya kuzaliwa, jambo lililoashiria kuzaliwa upya kwa roho safi na imani thabiti.
Mara tu alipomaliza kusoma Shahada, msikiti wa Hurghada ulijaa furaha na vilio vya “Allahu Akbar” (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa).
Waumini, katika tukio lililoakisi maana halisi ya undugu na ubinadamu, walimpongeza na kumuombea Muhammad awe na mafanikio na uthabiti katika imani yake mpya.
Sheikh Hussam Mahmoud, imamu na khatibu wa msikiti huo, alitaja tukio hilo kama kuzaliwa upya kwa mtu aliyechagua Uislamu kwa imani na hiari yake mwenyewe.
Tukio hilo liligeuka kuwa sherehe ndogo yenye roho ya uvumilivu na mapokezi ya watu wa Hurghada, wakimkaribisha raia huyo wa Argentina kwa mikono miwili, jambo lililoonyesha kuwa Uislamu ni dini ya wote dunaini na uwezo wa dini hii wa kuunganisha nyoyo za watu wa mataifa na makabila tofauti.
3494455