Akizungumza hivi karibuni katika sherehe za ufunguzi wa Msikiti wa Aali Ahmad (as) mjini Harare Zimbabwe, Hujjatul Islam wal Muslimeen Asadi Muwahhid alimwashiria Imam Khomeini (MA) kama mwanzilishi na mtetezi shupavu wa umoja na mshikamano wa Waislamu duniani na kusisitiza kwamba misikiti inapasa kutumiwa kama chombo muhimu cha kuunganisha na kuleta umoja miongoni mwa Waislamu.
Wapenzi na wafuasi wa Ahlul Bait (as) kutoka nchi za Lebanon, Iran na nchi nyingine za Asia walishiriki katika sherehe za ufunguzi wa msikiti huo.
Muwahhid ameongeza katika sherehe hizo zilizohudhuriwa na pia na Sayyid Akbar Pur Masoud, Naibu Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu wa Iran pamoja na mabalozi wa Iran, Indonesia na Pakistan kwamba, msikiti huo ni wa Waislamu wote wa Zimbabwe.
Akizungumzia nafasi ya misikiti katika kueneza Uislamu duniani, Bwana Pur Masoud amesema misikiti imekuwa na mchango mkubwa duniani na hasa katika mabara ya Afrika na Ulaya na kwamba kila mara maadui wanapotaka kutoa pigo dhidi ya Uislamu huilenga misikiti jambo ambalo amesema linaloonekana wazi katika sehemu nyingi za mabara hayo. 1058313