IQNA

Mkuu wa Baraza la Waislamu Ufaransa akutana na Rais wa nchi hiyo

22:45 - July 21, 2012
Habari ID: 2373997
Mkuu wa Baraza la Waislamu nchini Ufaransa Muhammad Mussawi amekutana na Rais wa nchi hiyo Francois Hollande mjini Paris.
Muhammad Mussawi alimshukuru Rais wa sasa wa Ufaransa kwa kutilia maanani masuala na matatizo ya Waislamu waliowachache nchini humo na akasema ana matumaini kwamba serikali mpya ya Paris itautambua Uislamu kuwa ni dini yenye taathira kubwa katika masuala ya kiroho ya nchi.
Mkuu wa Baraza la Waislamu nchini Ufaransa pia ametoa ripoti kuhusu shughuli za baraza hilo. 1058117
captcha