IQNA

Ujumbe wa makarii na mahafidhwa Misri wawasili Iran

22:45 - July 21, 2012
Habari ID: 2373998
Mshauri wa masuala ya Qur'ani wa kitengo cha masuala ya utamaduni cha Shirika la Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu la Iran amesema ujumbe wa makarii na mahafidh 77 kutoka Misri ambao unajumuisha walimu wa kiraa na hifdhi ya Qur'ani Tukufu umewasili nchini Iran sambamba na kuanza mwezi wa Ramadhani.
Ahmad Zarangar amesema kuwa ujumbe huo ambao umewasili nchini Iran kwa ushirikiano wa Kamati ya Masuala ya Qur'ani ya Shirika la Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu umealikwa katika kipindi cha Redio ya Jamhuri ya Kiislamu cha mapema kesho. Ameongeza kuwa ujumbe huo wa Misri ambao unajumuisha shakhsia mshuhuri wa masuala ya Qur'ani kama Ustadh Siddiq Mahmoud Minshawi, mwana wa Muhammad Siddiq Minshawi na Abdul Nasir Abdul Basit ambaye ni mtoto wa karii mashuhuri wa Misri Ustadh Abdul Basit utakuwa nchini Iran kwa kipindi cha wiki moja na katika muda huo utakuwa na ratiba mbalimbali zinazohusiana na kiraa ya Qur'ani Tukufu katika mwezi huu wa Ramadhani.
Zarengar amesema miongoni mwa ratiba hizo ni kutembelea Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanayoendelea mjini Tehran na kutembelea makao makuu ya Shirika la Habari la Kimataifa la Qur'ani IQNA. Vilevile utatembelea kituo cha kuchapisha Qur'ani cha Chuo cha Sayansi ya Qur'ani. 1058435
captcha