IQNA

Kitengo cha Utamaduni wa Waislamu katika Maonyesho ya Qur'ani Tehran

15:44 - July 22, 2012
Habari ID: 2374453
Kitengo cha 'Utamaduni na Mataifa ya Waislamu' katika Maonyesho ya 20 ya Kimataifa ya Qur'ani kimezinduliwa katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini RA mjini Tehran.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, nchi 25 zinaonyesha athari za Kiislamu na Qur'ani pamoja na sanaa za Qur'ani katika kitengo hicho.
Hussein Asadi Mkurugenzi wa Kitengo cha Qur'ani na Hadithi katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa chenye makao yake Qum, Iran amemwambia mwandishi wa IQNA kwa simu kuwa, kati ya nchi zinazoshiriki ni Pakistan, Thailand, India, Ivory Coast, Tanzania, Madagascar, Sudan, Tajikistan, Syria, Kosovo na Uturuki.
Mohammad Jara mkuu wa kibanda cha Ivory Coast amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa kati ya vitu alivyowasilisha katika maonyesho hayo ni nakala ya Qur'ani Tukufu iliyotarjumiwa kwa lugha ya Jula inayotumika sana nchini humo. Aidha anaonyesha kazi za kaligrafia pamoja na vitabu na majarida ya Kiislamu. Katika kibanda cha India kuna tarjumi za Qur'ani ya Kihindi, Kiurdu, Kinepal na Kigujarati.
Maonyesho ya 20 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanaendelea mjini Tehran katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini SA na yataendelea hadi tarehe 25 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
1058773
captcha