IQNA

Nchi za ASEAN kuchunguza mgogoro wa Myanmar

18:01 - July 23, 2012
Habari ID: 2374810
Mkutano wa kimataifa wa kuchunguza mauaji ya halaiki yanayofanywa dhidi y Waislamu wa Ruhigya nchini Myanmar unatazamiwa kufanyika tarehe 14 Agosti ukihudhuriwa na wanachama wa jumuiya hiyo ya mataifa ya Kusini mashariki mwa Asia (ASEAN).
Mkuu wa taasisi ya Ushirikiano wa Kiislamu wa Kimataifa ya Malaysia Zahidi Zainul Abidin amesema kuwa mkutano huo utakaoshirikisha taasisi za kiraia utafanyika hivi karibuni.
Amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kuunda makundi ya kutangaza maafa yanayowasibu Waislamu wa Myanmar.
Amesisitiza kuwa mkutano huo utakuwa hatua muhimu katika njia ya kuondoa hali ya kisikitisha ya Waislamu wan chi hiyo. 1058338

captcha