Ayatullah Akbar Hashimi Rafsanjani amesema mustakbali wa Palestina ni kadhia ya siku zote ya ulimwengu wa Kiislamu, kieneo na inayoihusu pia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Amesema anafurahishwa na kuimarika umoja na mshikamano kati ya makundi mbalimbali ya Wapalestina. Ayatullah Rafsanjani ameyasema hayo katika mazungumzo kati yake na Salah Zawawi Balozi wa Palestina mjini Tehran.
Mkuu wa Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel na dunia ya uistikbari zimekuwa zikifanya kila njama ili kuzusha migawanyiko na hitilafu kati ya makundi ya Wapalestina na katika ulimwengu wa Kiislamu.
1061132