Nils Muižnieks amezitaka serikali za nchi za Ulaya kufuta sheria zote na hatua zinazowalenga Waislamu kama sheria inayopiga marufu vazi la hijabu nchini Ufaransa.
Nils Muižnieks amesema kuwa serikali za Ulaya zinapaswa kufuta sheria na hatua zote zinazowalenga Waislamu na kupiga marufuku ubaguzi unaolenga dini au itikadi za watu katika nyanja zote.
Amesisitiza kuwa vyama vikubwa katika nchi za Ulaya vimetumia hisia za khofu zilizoenezwa dhidi ya Waislamu kuunga mkono sheria zinazowabana wafuasi wa dini hiyo. Ametolea mfano nchi za Ubelgiji na Ufaransa ambako sheria za nchi hizo zinawatoza faini wanawake wa Kiislamu wanaovaa nikabu katika maeneo ya umma.
Kamishna wa Haki za Binadamu wa Baraza la Ulaya anasema Waislamu barani humo wanakabiliana na aina mbalimbali ya ubaguzi na ukatili.
Uchunguzi uliofanywa hivi karibuni na Wakala wa Umoja wa Ulaya wa Haki za Binadamu pia ulibaini kuwa thuluthi moja ya Waislamu barani humo wamekumbana na vitendo vya kibaguzi katika miezi 12 iliyopita na kwamba robo ya Waislamu waliohusishwa katika uchunguzi huo wametiwa nguvuni na vyombo vya usalama mwaka uliopita. 1062231