Hizbullah imesema hatua hiyo imelenga kuanzisha vita vikubwa katika ardhi za Wapalestina kwa madhumuni ya kuwafukuza humo wamiliki wake halisi ili kuuwezesha utawala huo kuzidhibiti kwa nguvu.
Hizbullah imesema hatua hiyo ni jinai mpya ya Wazayuni dhidi ya Wapalestina na imeyataka mataifa ya Kiarabu na Kiislamu pamoja na jumuiya za kimataifa kutekeleza majukumu yao kwa kutetea haki za Wapalestina.
Hizbullah pia imelitaka taifa la Palestina lishikamane na thamani za mapambano na kulinda ardhi zake, hata kama jambo hilo litakuwa na changamoto nyingi.
Watetezi wa haki za binadamu walifichua siku ya Jumatatu iliyopita kwamba Wizara ya Ulinzi ya Israel imewafukuza mamia ya Wapalestina katika vijiji kadhaa vya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa kisingizio kwamba jeshi la utawala huo linahitajia eneo la kufanyia mazoei ya kijeshi. 1061887