IQNA

16:52 - July 28, 2012
Habari ID: 2378378

OIC yamtaka rais wa Myanmar kusitisha hujuma dhidi ya Waislamu

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) Profesa Ekmeleddin Ihsanoglu amemtumia barua Rais Thein Sein wa Myanmar na kumtaka asitishe hujuma na ukatili dhidi ya Waislamu wa kabila la Rohingya katika eneo la Arakan magharibi mwa pwani ya nchi hiyo.

Katika barua hiyo Ihsanoglu amesisistiza juu ya udharura wa kusitishwa mara moja ukatili dhidi ya Waislamu wa Myanmar na kusema matatizo yao yanapaswa kutatuliwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Ametoa wito kwa Rais Sein kuanzisha uchunguzi wa haraka kuhusu mauaji ya Waislamu wa kabila la Rohingya na kuwafikisha kizimbani wahusika.
Aidha Katibu Mkuu wa OIC amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kumtaka atumie ofisi yake kuwasaidia Waislamu wa Myanmar wanaokandamizwa.
Tokea mwezi Juni mwaka huu wa 2012, maelfu ya Waislamu wa kabila la Rohingya wameuawa na makumi ya maelfu ya wengine kuachwa bila makao kufuatia machafuko yaliyozuka mashariki mwa Myanmar.
Idadi ya Waislamu wa kabila la Rohingya ni karibu milioni moja kati ya watu milioni 47 katika nchi hiyo ya mashariki mwa Asia.
1063325
captcha