IQNA

Kitabu cha 'Ahlul Bait (as) katika Qur'ani na Hadithi' kwa lugha ya Kimalagasi chaonyeshwa Tehran

17:21 - July 28, 2012
Habari ID: 2378943
Kitabu kinachozungumzia Ahlul Bait wa Mtume (saw) kwa lugha ya Kimalagasi kinaonyeshwa katika maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanayoendelea mjini Tehran katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Akizungumza na shirika la habari za Qur'ani (IQNA) katika maonyesho hayo, Sakiri Mosimo, mkuu wa kibanda cha Madagascar katika maonyesho hayo amesema kwamba kitabu hicho kinaashiria aya za Qur'ani na hadithi za Mtume ambazo zinazungumzia ulazima wa kufuata uongozi wa Ahlul Bait (as).
Aya na hadithi zilizomo katika kitabu hicho zimetarjumiwa kwa lugha ya kimalagasi na Sheikh Badrudeen.
Vitabu vingine vinavyoonyeshwa kwenye kibanda hicho ni pamoja na tarjumi ya Qur'ani Tukufu iliyotarjumiwa kwa Kimalagasi na Akbar Ali Hanif na pia tarjumi ya dua ya Kumeil iliyotarjumiwa kwa lugha za Kifaransa na Kimalagasi na Taasisi ya Kiislamu ya Madagascar.
Waislamu wanaunda asilimia 10 ya jamii yote ya watu wa Madagascar ambapo asilimia 3 ya hao ni Mashia ambao wanaishi magharibi mwa nchi. 1063542
captcha