Kwa mujibu wa tovuti ya On Islam, Ahmad Gil mkuu wa jamii ya Kiislamu ya Augusta amesema kituo hicho kitakuwa daraja la kuwaunganisha wakazi Waislamu na wasio Waislamu wa mji huo kwa maana kwamba, milango ya kituo hicho itakuwa wazi kwa wasiokuwa Waislamu ili wapate kushirikiana na kubadilishana mawazo na Waislamu kuhusiana na masuala tofauti ya kidini na kiutamaduni. Amesema hatua hiyo itawawezesha wasiokuwa Waislamu kuufahamu vyema Uislamu.
Kituo hicho cha Kiislamu ambacho kina uwezo wa kubeba watu 1500 kina uwanja wa michezo na vyumba vya masomo. Marekani ina Waislamu wapatao milioni 7. 1055238