Gazeti la al Bayan linalochapishwa Imarati limeripoti kuwa, mashindano hayo yalianza jana usiku kwa mchuano wa makarii 8 kutoka nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu mbele ya majaji katika ukumbi wa ofisi za Chumba cha Biashara na Viwanda.
Miongoni mwa walioshiriki katika kikao cha siku ya kwanza ya mashindsano ya kimataifa ya Qur'ani ya Dubai ni Abbas Abdul Nasser kutoka Uingereza, Ainul Arifin kutoka Bangladesh, Hassan Katongoli kutoka Uganda na Omar Abdullah Salim kutoka Tanzania.
Kabla ya kuanza mashindano hayo kulifanyika vikao kadhaa vya mashindano hayo ambavyo vilimalizika Alkhamisi iliyopita. Vikao hivyo vilihutubiwa na maulamaa wa Kiislamu na wahubiri mashihuri kutoka nchi mbalimbali. 1063853