IQNA

Nakala ndogo zaidi ya Qur'ani yanakshiwa katika ukurasa wa fedha

18:59 - July 28, 2012
Habari ID: 2379319
Nakala ndogo zaidi ya Qur'ani Tukufu iliyotengenezwa na msanii Ranin Akbar Khanzadeh wa Iran imenakshiwa katika ukurasa mmoja nusu wa madini ya fedha wenye kipimo sawa na cha karatasi ya A4.
Kituo cha habari cha The Muslim Times kimeripoti kuwa, msaani Muirani Ranin Akbar Khanzadeh ambaye kwa sasa yuko Dubai amenakishi sura zote 114 za Qur'ani Tukufu katika ukurasa mmoja nusu wa fedha na kuweka rekodi nyingine katika uwanja huo.
Msanii huyo ana uwezo wa kuandika na kusoma herufi ndogo mara 30 zaidi kuliko herufi za kawaida ambazo haziwezi kusomwa na mtu mwingine bila ya kutumia chombo. Msanii huyo anatumia uwezo huo katika kuandika aya na sura za Qur'ani Tukufu na tangu miaka 12 iliyopita amekuwa akiandika nakala moja ya aina yake ya Qur'ani kila mwaka.
Msanii huyo wa Iran tayari amekwishaandika Qur'ani juu ya unyele na punje za mchele. Mpango wa baadaye wa msanii huyo ni kunakshi Qur'ani Tukufu juu ya madini ya thamani kama almasi na dhahabu. Kazi hiyo itakamilika mwezi Ramadhani mwaka ujao. 1064214
captcha