Kwa mujibu wa shirika la habari la Imarati WAM, kituo hicho kilifunguliwa wiki uliyopita sambamba na mashindano ya Qur'ani ya Zawadi ya Ajman.
Kituo hicho kitakuwa kikijishughulisha na masuala yanayohusiana na vitabu vya Kiislamu pamoja na turathi nyingine za Kiislamu.
Kituo hicho kilichoanzishwa kwa ushirikiano wa taasisi na jumuiya za Qur'ani kitajishughulisha pia na uenezaji wa mafundisho ya Qur'ani. Uchapishaji wa Qur'ani Tukufu na tarjumi zake kwa lugha tofauti ni miongoni mwa shughuli za kituo hicho. 1064817