Rashida Salimu, mratibu wa mashindano hayo amesema kwamba lengo la kuandaliwa mashindano hayo ni kunyanyua kiwango cha ufahamu wa wanafunzi kuhusiana na Uislamu na fadhila za mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Amefafanua kwamba jambo hilo litawawezesha wanafunzi kutafiti kuhusu jambo hilo na hivyo kuimarisha viwango vyao vya utambuzi wa mambo.
Amesema zawadi zitatolewa mwishoni mwa mwezi wa Ramadhani kwa wanafunzi watakaofanya vyema katika mashindano hayo.
Sehemu ya kwanza ya mashindano hayo ilifanyika Jumatano iliyopita na sehemu ya pili ambayo itahusiana na usomaji Qur'ani imepangwa kufanyika siku ya Jumanne ijayo. 1063959