IQNA

Maonyesho ya tatu ya kimataifa ya bidhaa halali kufanyika Uturuki

16:32 - July 29, 2012
Habari ID: 2380143
Maonyesho ya tatu ya kimataifa ya bidhaa halali na salama imepangwa kufanyika tarehe 11 hadi 14 Oktoba mjini Istanbul, Uturuki.
Katika maonyesho hayo watumiaji na wazalishaji wa bidhaa halali kutoka nchi zaidi ya 30 za Ulaya, Mashariki ya Kati, kaskazini mwa Afrika, mahariki ya mbali na Marekani watapata fursa ya kutambuana na wazalishaji wa bidhaa halali kote duniani.
Vilevile wazalishaji wenye kibali cha bidhaa halali watatangaza bidhaa zao na maonyesho hayo ni fursa nzuri ya kuanzisha uhusiano wa kibiashara kwa wazalishaji wa bidhaa halali.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa thamani ya soko la kimataifa la bidhaa halali ni dola trilioni mbili. 1064864
captcha