Sherehe za ufunguzi wa kituo hicho zimepangwa kuanza saa tatu na nusu usiku kwa wakati wa Tehran ambapo viongozi wa ngazi za juu wa masuala ya Qur'ani na utamaduni nchini wanatazamiwa kushiriki.
Bangladesh, Afghanistan, Russia, Ufilipino, Pakistan, Ghana, Algeria, Uturuki, Lebanon, Bosnia na Syria ni baadhi ya nchi za kigeni zinazoshiriki katika maonyesho hayo. Kitengo hicho cha kimataifa kitafunguliwa kwa muda wa siku 10 ambapo watafiti, waandishi na wachapishaji wa Qur'ani Tukufu na vitabu vingine vinavyohusiana na kitabu hicho kitakatifu kutoka nchi za kigeni watawasilisha kazi zao. Wasomi, wasanii na shakhsia wa Qur'ani kutoka nchi tofauti za dunia wamealikwa kushiriki katika shughuli za kitengo hicho.
Kitengo hicho kimepata umuhimu maalumu hasa katika kipindi hiki ambapo nchi nyingi za Kiislamu zinashuhudia wimbi la mwamko wa Kiislamu.
Wasimamizi wa kitengo hicho wanasema kuakisiwa shughuli za Qur'ani za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nje ya nchi ni miongoni mwa malengo muhimu ya kituo hicho. 1065240