IQNA

Maandamano ya kupinga mashambulizi dhidi ya Msikiti wa al Aqsa yafanyika Jordan

16:07 - July 30, 2012
Habari ID: 2381088
Makundi mbalimbali ya vijana wa Jordan jana usiku yalikusanyika mbele ya Wizara ya Wakfu ya nchi hiyo na kutangaza upinzani wao dhidi ya wito uliotolewa na utawala ghasibu wa Israel wa kushambuliwa Msikiti wa al Aqsa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Waandamanaji hao wamewataka viongozi wa serikali ya Jordan kuchukua msimamo imara dhidi hatua hiyo ya utawala ghasibu wa Israel.
Waandamanaji hao pia walipiga nara zinazoitaka serikali ya Amman kuchukua hatua za haraka za kuzuia mashambulizi ya Wayahudi dhidi ya Msikiti wa al Aqsa katika siku inayoitwa "siku ya kuharibiwa maabadi.
Vilevile wametahadharisha kwamba iwapo serikali ya Jordan itanyamaza kimya watadumisha maandamano hayo.
Kwa mujibu wa makubaliano ya amani yaliyotiwa saini kati ya Jordan na utawala wa Kizayuni wa Israel, serikali ya Amman ilipewa jukumu la kulinda maeneo matakatifu ya Palestina hususan Msikiti wa al Aqsa. 1066099


captcha