Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kikao hicho kilihudhuriwa na Sheikh Zaghloul, Sayyed Baqir, Sayyid Javadi mkuu wa idara ya utamauni Iran nchini Nigeria.
Akihutubia kikao hicho, Sayyid Javadi, amezungumzia fadhila za Ahlul Bayt AS pamoja na utakasaji wa nafsi katika mwezi huu mtukufu pamoja na umuhimu wa dua kwa mtazamo wa Ahlul Bayt AS.
Huku akiashiria namna Qur’ani Tukufu ilivyosisitiza juu ya suala la udugu, amesema umoja ni hitajio la dharura katika jamii za Kiislamu.
1065765