IQNA

Mashindano ya Qur’ani yafanyika Qatif Saudi Arabia

17:00 - July 31, 2012
Habari ID: 2381435
Mashindano ya saba ya tajweed na kuhifadhi Qur’ani Tukufu yamefanyika Qatif katika mkoa wa mashariki mwa Saudi Arabia.
Mashindano hayo yaliyofanyika Julai 27 yameandaliwa na kituo cha Darul Quran.
Kwa mujibu wa tovuti ya Walfajr, mashindano hayo yameandaliwa kama sehemu ya Tamasha ya 19 ya Misaada katika eneo la Hai al Bir mjini Qatif.
Washiriki 26 wakiwemo vijana na watoto walishiriki katika mashindano hayo yaliyojumuisha kuhifadhi juzu Amma, Suratul Jumu’a na Insan na vilevile tajweed ya Qur’ani Tukufu.
Msimamizi wa mashindano ya mwaka huu Murtadha As Sayyid Salhe amesema majaji walikuwa wataalamu wa Qur’ani kama vile Muhammad Abu Sa’eed, Adel Al Javad, na Issa Abu Sa’eed.
Walioshinda watatunukiwa zawadi katika sherehe itakayofanyika Agosti 6.
1065002
captcha