IQNA

Qur'ani zatawanywa Palestina

17:07 - July 31, 2012
Habari ID: 2381818
Kamati ya Mawasiliano ya Umma na Marekebisho inayofungamana na Chama cha Jihadul Islami cha Palestina imesambaza nuskha za Qur'ani Tukufu kwa wakazi wa mji wa Rafah katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
Kwa mujibu wa gazeti la Palestina la Dunia al-Watan kamati hiyo imekuwa ikitoa nakala hizo za Qur'ani kwa wakazi wa mji uliotajwa tokea mwanzoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Lengo la kusambazwa Qur'ani hizo limetajwa kuwa ni kuwashajiisha wakazi wa mji huo wajishughulishe zaidi na suala la usomaji kitabu hicho kitakatifu na kutekeleza mafundisho yake maishani.
Akifafanua suala hilo, Sheikh Abul Adib ad-Durbi mkuu wa kamati hiyo amesema kwamba kutoa umuhimu kwa nafasi ya Qur'ani katika jamii ya Kiislamu na kufanyika juhudi za kutekeleza mafundisho yake ni malengo muhimu ya kutekelezwa mpango wa kutolewa Qur'ani hizo kwa familia za Palestina katika mji wa Rafah. 1066285
captcha